Hamia kwenye habari

AGOSTI 8, 2019
UFARANSA

Paris, Ufaransa—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

Paris, Ufaransa—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
  • Tarehe: Agosti 2-4, 2019

  • Mahali: Parc des Expositions de Paris-Nord Villepinte huko Paris, Ufaransa

  • Lugha ya Programu: Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kijerumani, Kiromania, na Kirusi

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 37,809

  • Idadi ya Waliobatizwa: 265

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,500

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Chile, Côte dʹIvoire, Ekuado, Kanada, Kazakhstan, Marekani, Moldova, New Caledonia, Tahiti, Ugiriki, Uingereza, Ulaya ya Kati, Zambia

  • Mambo Yaliyoonwa: Meneja mmoja wa sehemu ambayo kusanyiko lilifanyiwa, alipoona foleni ya magari aliuliza: “Kwani ninyi watu hamkasiriki? Wakati wa kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, hakuna mtu aliyepiga honi, hakukuwa na madereva wajeuri, hakuna mtu aliyeonekana amekasirika, wala hakuna mtu aliyekatiza kwenye foleni.”

    Mfanyakazi mmoja kwenye hoteli iliyotumiwa na wajumbe alisema: “Nimeona vikundi vingi, lakini shirika lenu ndilo shirika bora kuliko mashirika yote. Watu walionekana kuwa na furaha na kulikuwa na uchangamfu sana!”

Ndugu na dada wenyeji wakiwakaribisha wajumbe kwenye uwanja wa ndege huko Paris

Ndugu na dada wakishiriki katika mahubiri ya hadharani; Mnara maarufu wa Eiffel unaonekana kule nyuma

Ndugu na dada wakizungumza nje ya eneo la kusanyiko

Mwanamume na mke wake walibatizwa pamoja siku ya Jumamosi

Wajumbe wa kimataifa waliovalia mavazi ya kitamaduni ya Tahiti wakisikiliza programu ya kusanyiko

Ndugu Anthony Morris, mshiriki wa Baraza Linaloongoza akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumamosi

Watumishi wa pekee wa wakati wote wanaonekana kwenye skrini, wakiwapungia watu mkono mwishoni mwa programu ya Jumapili

Ndugu akionyesha jinsi ya kuoka mikate ya kitamaduni ya Ufaransa katika Betheli