Asubuhi ya Agosti 14, 2017, mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliharibu maduka, barabara, na nyumba kotekote jijini Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone. Zaidi ya watu 400 wamekufa na wengine 600 hawajulikani walipo. Maofisa wanahofia kwamba mvua ambazo bado zimetaribiwa kutokea zitasababisha uharibifu.

Ofisi ya tawi ya Sierra Leone inaripoti kwamba hakuna Shahidi wa Yehova aliyekufa au kujeruhiwa wakati wa janga hili. Hata hivyo, familia mbili zimeachwa bila makao. Wazee wa makutaniko ya eneo hilo wanawaandalia Mashahidi wenzao uchungaji wa kiroho. Isitoshe, wazee wamekuwa wakisambaza habari inayoonyesha tahadhari za kuchukua iwapo mafuriko zaidi yatatokea.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Sierra Leone: Collin Attick, +232-76-67-90-75