Mvua kubwa kusini-magharibi ya Nigeria iliyoanza Julai 6 hadi Julai 12, 2017, ilisababisha mafuriko katika majimbo ya Lagos, Niger, na Oyo. Vyombo vya habari vilieleza kwamba watu 18 hivi wamekufa kwa sababu hiyo.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Nigeria imethibitisha kwamba hakuna Mashahidi wa Yehova waliojeruhiwa au kufa wakati wa tukio hilo, ingawa wanne kati yao walilazimika kuhama. Isitoshe, nyumba mbili za Mashahidi ziliathiriwa na moja ikaharibiwa kabisa. Mashahidi nchini Nigeria wanaandaa msaada kwa waabudu wenzao na pia majirani ambao si Mashahidi, ambao baadhi yao walilazimika kuhama au nyumba zao ziliharibiwa.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Nigeria: Paul Andrew, simu +234-7080-662-020