Septemba 19, 2017, tetemeko kubwa la nchi lilipiga eneo la Mexico ya Kati, na kuua watu zaidi ya 200. Tumepata habari ifuatayo kutoka ofisi ya tawi ya Amerika ya Kati.

Inasikitisha kwamba dada mmoja jijini Mexico City alikufa wakati wa tetemeko hilo. Pia, dada mmoja hajulikani alipo baada ya jengo alilokuwa akiishi kuanguka. Katika jiji la Puebla, dada mmoja alijeruhiwa vibaya, na katika Jimbo la Mexico, dada mwingine alilazwa hospitalini kwa sababu ya majeraha.

Ilibidi Wanabetheli wahame kutoka ofisi ya tawi kwa muda fulani lakini sasa wamerudia shughuli za kawaida. Hakuna yeyote aliyejeruhiwa na majengo hayakuharibiwa.

Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu katika kipindi hiki kigumu tukijua kwamba Yehova atawategemeza na anaelewa vema “mateso” yao.—Zaburi 31:7.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52-555-133-3048