Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 20, 2017
MEXICO

Kimbunga Max Kimepiga Kusini ya Mexico

Kimbunga Max Kimepiga Kusini ya Mexico

Septemba 14, 2017, pwani ya Pasifiki kusini ya Mexico ilipigwa na Kimbunga Max, ambacho mwishowe kilipungua nguvu na kuwa dhoruba. Kimbunga hicho kilisababisha upepo mkali na mvua iliyotokeza mafuriko yenye madhara.

Bado uchunguzi unaendelea kuhusu madhara yaliyosababishwa. Hata hivyo, inasikitisha ndugu yetu mmoja alikufa wakati wa kimbunga hicho alipokuwa akijaribu kumwokoa jirani yake. Ofisi ya tawi nchini Mexico inasimamia kazi ya kutoa msaada na inafanya kazi na makutaniko ya eneo hilo ili kuwategemeza wale walioathiriwa na kimbunga.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52-555-133-3048