Hamia kwenye habari

JUNI 20, 2019
MEXICO

Monterrey, Mexico—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”

  • Tarehe: Juni 7-9, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa BBVA Bancomer wa Monterrey, Mexico

  • Lugha ya Programu: Kiingereza, Lugha ya Ishara ya Mexico, Kihispania

  • Maeneo Yaliyounganishwa: 38 katika nchi 6 (Kosta Rika, Guatemala, Honduras, Mexico, Nikaragua, na Panama)

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 39,099

  • Idadi ya Waliobatizwa: 393

  • Idadi wa Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 4,682

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Argentina, Brazili, Kolombia, Ufaransa, Italia, Japani, Uholanzi, Paraguai, Peru, Hispania, Marekani

  • Mambo Yaliyoonwa: Roberto Valero, mwakilishi wa meya katika jiji la Guadalupe, alitembelea eneo la kusanyiko siku ya Jumamosi. Kati ya mambo mengine, alisema hivi: “Serikali imeazimia kudumisha amani na usalama wa watu wake. Na ninyi Mashahidi wa Yehova, mmechangia sana kwa kuwa raia wema. Jiji zima linatambua hilo.”

 

Ndugu na dada wakiwakaribisha wajumbe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Monterrey

Wajumbe wakifika kusanyikoni, Mlima Silla unaovutia unaonekana upande wa nyuma

Ndugu Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Ijumaa

Mtu akibatizwa Jumamosi katika moja ya vidimbwi vinne vilivyotumiwa kusanyikoni

Wajumbe wa mataifa mbalimbali wakisikiliza kwa makini programu ya kusanyiko

Watumishi wa pekee wa wakati wote wakiwapungia watu mkono siku ya mwisho ya kusanyiko

Familia kutoka Apodaca, Mexico, wakiwa wameshika bango linalosema, ‘Tunawapenda’

Mjumbe na dada mwenyeji wakihubiri katika eneo la Monterrey

Wajumbe wafurahia dansi kutoka Mexico kaskazini inayoitwa Polka Norteña

Dada wakicheza dansi ya kitamaduni ya jimbo la Jalisco, Mexico