Januari 9, dhoruba kali ilipiga maeneo ya kusini ya California, Marekani na kutokeza maporomoko ya ardhi na uharibifu mkubwa kwa wakaaji wa maeneo hayo. Ripoti za habari zinaonyesha kwamba watu 21 hivi walikufa na mamia ya nyumba kuharibiwa.

Hakuna mhubiri aliyekufa kutokana dhoruba hiyo. Katika eneo la Burbank, nyumba na mali ya mhubiri mmoja ziliharibiwa, na katika eneo la Ventura familia nyingine nane zilihamishwa kutoka nyumbani kwao. Hakuna Majumba ya Ufalme yaliyoharibiwa na maporomoko hayo ya ardhi.

Waangalizi wa mzunguko na Halmashauri ya Kutoa Msaada Wakati wa Misiba, pamoja na wawakilishi wa Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi, wanaendelea kuwategemeza wahubiri walioathiriwa na maporomoko hayo ya ardhi na pia kutokana na mioto ya msituni inayoenea upesi. Tunaendelea kuwakumbuka ndugu zetu katika sala katika kipindi hiki, tukiwa na uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwaimarisha.—1 Petro 5:10.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000