Hamia kwenye habari

AGOSTI 15, 2019
MAREKANI

Phoenix, Marekani—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

Phoenix, Marekani—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
  • Tarehe: Agosti 9-11, 2019

  • Mahali: Chase Field, Phoenix, Arizona, Marekani

  • Lugha ya Programu: Kiingereza

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 40,237

  • Idadi ya Waliobatizwa: 352

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Uingereza, Kanada, Ulaya ya Kati, Chile, Ufaransa, Ugiriki, India, Italia, Korea, Micronesia, Skandinavia, Sri Lanka, Tahiti, Thailand, Trinidad na Tobago, Uturuki

  • Mambo Yaliyoonwa: Steve Moore, rais na mkurugenzi wa kampuni ya Visit Phoenix, ambayo ilisaidia kupanga makusanyiko na hoteli katika eneo la Phoenix alisema hivi: “Kwa muda mrefu ambao nimefanya kazi hii, [kusanyiko hili] ndilo kusanyiko pekee ambalo mambo yalifanywa kwa utaratibu mzuri sana. Nimefurahia sana kufanya kazi nanyi. Na pamoja na mambo hayo yote, mliahidi kwamba mngesafisha uwanja kabla ya kuondoka—hakuna mtu yeyote anayefanya hivyo.”

 

Wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakikaribishwa kwa uchangamfu walipofika kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sky Harbor jijini Phoenix

Ndugu na dada kutoka Phoenix wakiwa tayari kuwapokea wajumbe kwenye mojawapo ya hoteli

Mamia ya ndugu na dada wakiwasalimu wajumbe kwa shauku walipowasili kwenye uwanja wa kusanyiko wa Chase Field siku ya Ijumaa asubuhi

Wajumbe, baadhi yao wakiwa wamevaa mavazi ya asili wakisikiliza programu

Wahubiri wawili wapya kati ya 352 waliobatizwa

Ndugu Samuel Herd, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho katika siku ya pili ya kusanyiko

Wajumbe wakipiga picha walipotembelea hifadhi ya taifa

Ndugu zetu wakiwa ndani ya gari linalokokotwa na farasi ikiwa sehemu ya maonyesho ya kihistoria ya mji wa karne ya 19 wa Amerika ya Kaskazini

Watumishi wa wakati wote waliofika kwenye kusanyiko hilo wakitembea uwanjani baada ya programu kwisha Jumapili jioni