Hamia kwenye habari

JULAI 12, 2019
MAREKANI

Miami, Marekani (Kiingereza)—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe!”

  • Tarehe: Julai 5-7, 2019

  • Mahali: Marlins Park Miami, Florida, Marekani

  • Lugha za Programu: Kiingereza, Kichina cha Mandarini

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 28,000

  • Idadi ya Waliobatizwa: 181

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Brazili, Uingereza, Kanada, Kolombia, Jamhuri ya Dominika, Fiji, Ghana, Ugiriki, Hong Kong, Israel, Japani, Uholanzi, Skandinavia, Afrika Kusini, Hispania, Taiwan, Trinidad na Tobago, Ukrainia

  • Mambo Yaliyoonwa: Francis X. Suarez, meya wa jiji la Miami, alitembelea eneo la kusanyiko Jumapili na kusema: “Nimependa ujumbe unaowasilishwa, ‘Upendo Haushindwi Kamwe’!” Kisha aliongezea kwa kusema: “Ni ujumbe mzuri sana, nafikiri kusanyiko kama hili ni zuri sana kwa mji wowote mkubwa uliopo Marekani au popote duniani.”

 

Watoto wakisaidia kuwakaribisha wajumbe kwenye uwanja wa ndege wa Miami

Wajumbe wakishirikiana na wenyeji kukaribisha majirani kusanyikoni

Wajumbe wakipokea nakala za Tafsiri ya Ulimwengu Mpya iliyorekebishwa katika Kichina, ambayo ilitolewa siku ya Ijumaa

Wajumbe wakiandika mambo makuu kusanyikoni

Dada watatu kati ya ndugu na dada 181 wakibatizwa

Ndugu na dada wenyeji wakiwasalimia wajumbe na kupeana zawadi

Wamishionari na wanabetheli wanaotumikia katika nchi za kigeni wakiwapungia mkono wahudhuriaji siku ya Jumapili alasiri

Ndugu Lösch akisalimia watumishi wa wakati wote siku ya Jumapili

Watoto wakiwaburudisha wajumbe kwa wimbo wakati wa tafrija ya jioni