Hamia kwenye habari

JULAI 19, 2019
MAREKANI

Houston, Marekani (Kiingereza)—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe!”

  • Tarehe: Julai 12-14, 2019

  • Mahali: Uwanja wa michezo wa NRG ulio Houston, Texas, Marekani

  • Lugha ya Programu: Kiingereza, Kikorea

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 50,901

  • Idadi ya waliobatizwa: 401

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Ubelgiji, Brazili, Uingereza, Kanada, Kolombia, Czech-Slovak, Ufaransa, India, Italia, Japani, Korea, Filipino, na Skandinavia

  • Mambo Yaliyoonwa: Sylvester Turner, meya wa jiji la Houston, alistaajabu sana kuwaona Mashahidi wa Yehova 50,000 na wageni wao waliokwenda jijini Houston kwa ajili ya kusanyiko. Alisema hivi: “Ni kama kukaribisha hewa safi katika njia nyingi. Ndio maana tunafungua milango yetu. Ikiwa nyinyi [Mashahidi wa Yehova] mnaweza kuja mara mbili kwa mwaka, tunawakaribisha sana katika jiji hili la Houston. Mrudi mwaka ujao, na hata mwaka unaofuata.”

 

Ndugu na dada wakiwakaribisha wajumbe Houston

Wajumbe wakihubiri pamoja na wenyeji

Baadhi ya waliobatizwa kati ya ndugu na dada zetu wapya 401

Ndugu Anthony Morris, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba yake ya mwisho Jumamosi

Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali, wakipiga picha na baadhi yao wamevaa mavazi ya nchi waliyotoka

Wajumbe wakifurahia ushirika

Watumishi wa wakati wote wakipigiwa makofi wakati wa hotuba ya kumalizia ya Jumapili

Ndugu na dada wenyeji wakiwa jukwaani wakihitimisha tafrija ya jioni iliyotia ndani kuimba, kucheza dansi na historia fupi ya Mashahidi wa Yehova jijini Houston