Hamia kwenye habari

AGOSTI 30, 2019
MAREKANI

Houston, Marekani (Kihispania)—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

  • Tarehe: Agosti 23-25, 2019

  • Mahali: Uwanja wa NRG huko Houston, Texas, Marekani

  • Lugha ya Programu: Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 56,167

  • Idadi ya Waliobatizwa: 626

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,500

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Amerika ya Kati, Argentina, Bolivia, Chile, Ekuado, Hispania, Italia, Jamhuri ya Dominika, Japani, Kolombia, Peru, Trinidad na Tobago, Ufaransa, Ufilipino, Venezuela

  • Mambo Yaliyoonwa: Joelle Hardin, meneja wa mauzo na usimamizi wa mipango katika kampuni ya Space Center Houston, alisema: “Leo asubuhi, mmoja wa wafanyakazi wangu [aliyekuwa akihakiki tiketi za wajumbe walipokuwa wakiingia katika jengo] alinijia na kuniambia, ‘Joelle, . . . kila mmoja wao alinitazama usoni na kuniambia, “Asante,” wengine waliniambia kwa lugha ya kigeni.’ Hilo lilimfurahisha sana. Kwa muda fulani sijamwona akiwa amechangamka hivyo.”

 

Wajumbe wakiwasili kwenye uwanja wa michezo asubuhi

Wajumbe wakihubiri pamoja na ndugu na dada wenyeji

Maelfu ya wajitoleaji wakishiriki kusafisha uwanja wa michezo wa NRG kabla ya programu kuanza siku ya Ijumaa

Wawili kati ya ndugu na dada 626 waliobatizwa

Ndugu Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho Ijumaa alasiri

Wajumbe wakisikiliza na kuandika mambo makuu ya programu

Dada akitembeza kikundi cha wageni kwenye Makumbusho ya Sayansi Asilia huko Houston, mojawapo ya matembezi yaliyopangwa kwa ajili ya wajumbe

Ndugu na dada zetu wakiwatumbuiza wajumbe katika tafrija ya jioni

Watumishi wa pekee wa wakati wote wakipungia mkono kamera kutoka uwanjani mwishoni mwa programu ya siku ya Jumapili