Januari 27, 2019, tufani ilipiga eneo la Havana, mji mkuu wa nchi ya Kuba. Kasi ya upepo ilifikia kilomita 322 kwa saa, na hivyo kufanya tufani hiyo kuwa dhoruba kubwa zaidi kupiga kisiwa hicho kwa miaka karibu 80. Tufani hiyo iliathiri eneo la kilomita 11 hivi na kuharibu majengo na kusababisha mafuriko. Watu 4 wamekufa, na wengine 195 wamejeruhiwa.

Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa kutokana na dhoruba hiyo. Hata hivyo, nyumba 26 zimeharibiwa kwa kiwango fulani, 3 kati ya hizo zinatumiwa kwa ajili ya mikutano ya kutaniko. Mipango inafanywa ili kazi ya kukarabati ianze.

Waangalizi wa mzunguko wamekuwa wakiwategemeza kiroho waabudu wenzao ambao wamevumilia tufani hiyo na madhara iliyosababisha. Tunasali kwamba Yehova atawapa ndugu na dada zetu amani wanapokabiliana na janga hilo.—Hesabu 6:26.