Hamia kwenye habari

APRILI 11, 2018
KAZAKHSTAN

Teymur Akhmedov Ameachiliwa Huru Kutoka Gerezani Nchini Kazakhstan Aprili 4, 2018

Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan alimwondolea mashtaka yote Teymur Akhmedov, na Aprili 4, 2018 akaachiliwa huru kutoka kifungoni. Machi 27, 2018, wenye mamlaka walimruhusu Ndugu Akhmedov afanyiwe upasuaji wa dharura katika hospitali huko Almaty, ambapo bado anaendelea kupata nafuu.

Ndugu Akhmedov, mwenye umri wa miaka 61, amekuwa gerezani tangu Januari 18, 2017, kwa sababu tu ya kushiriki ibada. Amefurahi sana kwamba hatimaye ameungana tena na familia yake.

Tunashangilia kwamba Yehova alimkomboa mtumishi wake mshikamanifu.—2 Samweli 22:2.