Msimu wa mvua ndefu umesababisha dhoruba kali za radi na mvua kubwa zaidi ambayo haijawahi kutokea nchini India kwa zaidi ya karne moja. Majimbo kadhaa yameathiriwa na mafuriko na maporomoko ya nchi; na watu 700 hivi wamekufa na mamilioni ya watu wamepoteza makao.

Kufikia Julai 31, 2017, hakukuwa na Shahidi wa Yehova aliyejeruhiwa au kufa. Hata hivyo, nyumba za familia angalau tatu za Mashahidi zilijawa na maji ingawa hazikuharibika sana. Makutaniko ya Mashahidi wa Yehova nchini India yanaandaa msaada unaofaa kwa waabudu wenzao.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

India: Tobias Dias, simu +91-9845476425