Hamia kwenye habari

JULAI 26, 2019
HISPANIA

Madrid, Hispania—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe!”

  • Tarehe: Julai 19-21, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa Wanda Metropolitano ulioko Madrid, Hispania

  • Lugha ya Programu: Kiingereza, Kihispania, Lugha ya Ishara ya Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 52,516

  • Idadi ya Waliobatizwa: 434

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,300

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Albania, Argentina, Bulgaria, Kanada, Amerika ya Kati, Jamhuri ya Dominika, Ghana, Hungaria, Korea, Uholanzi, Peru, Slovenia, Taiwan, Uturuki, Marekani

  • Mambo Yaliyoonwa: César López, mkurugenzi wa makao katika moja ya hoteli ambazo wajumbe walikaa alisema: “Tumejionea mambo ambayo si ya kawaida katika kipindi hiki. Moja kati ya vitu ambavyo wafanyakazi wetu hawakuacha kuzungumzia ni jinsi watu waliohudhuria tukio hili walivyokuwa—tabasamu lao, mwenendo wao mzuri na urafiki waliokuwa nao. Nafikiri ujumbe wenu [“Upendo Haushindwi Kamwe”] ni jambo ambalo wajumbe hawa walijifunza kabla ya kuja hapa. Ulionyeshwa na kila mtu aliyekaa hotelini kwetu. Tungependa kuwakaribisha wajumbe wenu wakati mwingine tena.”

 

Ndugu na dada wenyeji wakiwasalimia kwa shauku wajumbe waliofika katika uwanja wa ndege wa Adolfo Suárez Madrid-Barajas

Dada mwenyeji akihubiri pamoja na mjumbe jijini Madrid wakitoa mialiko ya kusanyiko

Wajumbe wengi wakiingia uwanja wa kusanyiko wakati wa kipindi cha asubuhi

Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakitabasamu na kupungia mwishoni mwa programu ya Ijumaa

Vijana wawili Mashahidi katika moja kati ya maeneo yaliyounganishwa wakionyesha vifaa vyao vyenye nakala ya kielektroni ya Biblia iliyorekebishwa ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya katika lugha ya Kihispania. Biblia hiyo ilitolewa wakati uleule Madrid na sehemu nyingine 11 nchini Hispania siku ya Ijumaa

Mmoja kati ya ndugu na dada wapya 434 akitabasamu baada ya kubatizwa

Watumishi wa pekee wa wakati wote wakiwapungia ndugu na dada wakiwa wamesimama uwanjani siku ya mwisho ya kusanyiko

Ndugu na dada wakipiga makofi kwa shangwe kusanyikoni

Ndugu Gerrit Lösch, mshiriki wa Baraza Linaloongoza akisalimiana na mmoja wa watumishi wa pekee wa wakati wote mwishoni mwa kusanyiko

Akina dada wakiwa wamevaa mavazi mazuri yenye rangi wakiwa wanacheza dansi ya asili ya Kihispania kwenye tafrija ya jioni