Hamia kwenye habari

MACHI 16, 2021
Guinea ya Ikweta

Milipuko Mibaya Yatokeza Uharibifu na Huzuni Nchini Guinea ya Ikweta

Milipuko Mibaya Yatokeza Uharibifu na Huzuni Nchini Guinea ya Ikweta

Eneo

Mondong Nkuantoma katika jiji la Bata, Guinea ya Ikweta

Janga

 • Machi 7, 2021, milipuko kadhaa ilitokea kwenye kambi ya jeshi katika jiji kubwa zaidi nchini Guinea ya Ikweta. Milipuko hiyo ilitokeza uharibifu mkubwa sana

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

 • Wahubiri 12 wamepata majeraha madogo

 • Wahubiri 42 wamelazimika kuhama makazi yao

 • Binti mwenye umri wa miaka 9 wa dada mmoja yuko katika hali mbaya

 • Baadhi ya wahubiri wamewapoteza watu wa ukoo ambao si Mashahidi katika kifo

Uharibifu wa mali

 • Nyumba 23 ziliharibiwa kidogo

 • Nyumba 6 zilipata uharibifu mkubwa

 • Nyumba 6 zimeharibiwa kabisa

Jitihada za kutoa msaada

 • Halmashauri ya Kutoa Msaada ilianzishwa ili kuratibu jitihada za kutoa msaada na inafanya kazi pamoja na waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo ili kukagua madhara na mahitaji ya ndugu na dada

 • Pia, waangalizi wa mzunguko wanafanya kazi na wazee kuwaandalia wahubiri msaada wa kiroho

 • Jitihada zote za kutoa msaada zinapatana na miongozo ya usalama ya COVID-19

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwa kimbilio la ndugu na dada walioathiriwa na msiba huu.—Zaburi 46:1.