Hamia kwenye habari

NOVEMBA 12, 2020
FILIPINO

Vimbunga Viwili Vyashambulia Maeneo Mengi Nchini Filipino

Vimbunga Viwili Vyashambulia Maeneo Mengi Nchini Filipino

Mahali

Kusini mwa Luzon na visiwa vinavyoizunguka

Janga

  • Oktoba 25, 2020, Kimbunga Molave, kilichoitwa pia Quinta nchini Filipino kilipiga kijiji cha Albay kilicho katika mkoa wa Bicol ulio Luzon, Filipino. Upepo huo mkali ulivuma katika kisiwa chote cha Luzon

  • Novemba 1, 2020, Kimbunga Goni kilichokuwa na kasi sana, kilipewa jina Rolly nchini Filipino, kilipiga kisiwa cha Catanduanes katika mkoa wa Bicol ulio Luzon. Kimbunga hicho kiliendelea kuvuma hadi kwenye vijiji vingine, hadi vile ambavyo vilikuwa vimeathiriwa na Kimbunga Molave

  • Vimbunga hivyo viwili vilileta mvua kubwa na upepo mkali ambao ulisababisha mafuriko makubwa pamoja na ukosefu wa umeme na maji. Kuwasiliana na watu walio katika maeneo hayo ni vigumu sana

  • Mvua hizo kubwa zimesababisha pia lahars au matope yanayokuja na mabaki ya volcano ya Mlima Mayon ambayo yameharibu nyumba za watu wanaoishi karibu na mlima huo.

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri wengi wamepoteza makao au kulazimika kuhama makao yao

  • Dada mwenye umri wa miaka 89 alijeruhiwa kidogo alipokuwa akikimbia kutoka katika nyumba yake ambayo iliharibiwa kabisa

Uharibifu wa mali

  • Nyumba 134 na Majumba ya Ufalme 8 yalipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 75 na Majumba ya Ufalme 8 yaliharibiwa kwa kadiri ndogo

  • Nyumba 101 na Jumba ya Ufalme 1 liliharibiwa kabisa

Jitihada za kutoa msaada

  • Waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa wanashirikiana na Halmashauri 6 za Kutoa Msaada ili akina ndugu wapate chakula, maji, mahali pa kuishi na mahitaji mengine ya lazima. Ndugu zetu wanafuata kwa makini miongozo ya jinsi ya kujilinda na ugonjwa wa COVID-19

Tutaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu ambao wameathiriwa na majanga haya ya asili. Katika kipindi hiki kigumu, tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwa “Baba wa rehema nyororo na Mungu wa faraja yote” kwa ndugu na dada zetu.—2 Wakorintho 1:3.