Hamia kwenye habari

JANUARI 20, 2020
FILIPINO

Mlima wa Volkano Nchini Filipino Warusha Majivu Kukiwa na Hatari ya Kulipuka

Mnamo Januari 12, 2020, mlima wa volkano wa Taal huko Batangas, Filipino, ulirusha majivu kufikia kilomita 14 angani, na maonyo yakatolewa kuhusu uwezekano wa “mlipuko unaoweza kusababisha vifo.” Wenye mamlaka wameagiza maelfu ya watu wanaoishi karibu na mlima huo wahame kabisa.

Kufikia sasa, zaidi ya akina ndugu 500 wamehamishiwa kwenye maeneo salama kutia ndani Majumba ya Ufalme na nyumba za Mashahidi wengine. Hakuna yeyote kati ya ndugu zetu aliyejeruhiwa. Halmashauri ya Tawi imeteua Halmashauri ya Kutoa Misaada ili kushughulikia mahitaji ya msingi ya wale waliohamishwa.

Tunasali kwamba ndugu na dada zetu nchini Filipino wataendelea kumtegemea Yehova, “kimbilio letu na nguvu zetu.”—Zaburi 46:1-3.