Hamia kwenye habari

JANUARI 2, 2020
FILIPINO

Kimbunga Phanfone Chapiga Filipino

Kimbunga Phanfone, ambacho pia kinaitwa kimbunga Ursula, kilipiga Filipino Desemba 24, 2019, katika mkoa wa Samar Mashariki. Hakuna Shahidi wa Yehova hata mmoja aliyekufa au kujeruhiwa. Hata hivyo, nyumba 464 za Mashahidi ziliharibiwa kutia ndani Majumba 6 ya Ufalme. Ofisi ya Tawi ya Filipino imeunda Halmashauri tano za Kutoa Msaada ili ndugu zetu wapewe msaada wa kiroho na wa kimwili katika visiwa kadhaa vilivyoathiriwa na msiba huo.

Kimbunga Phanfone kilikuwa kimbunga cha 21 kupiga Filipino katika mwaka wa 2019. Pia hivi karibuni matetemeko ya ardhi yamekuwa yakipiga kusini mwa nchi hiyo. Hivyo, kufikia sasa, jumla ya Halmashauri 18 za Kutoa Msaada zinafanya kazi.

Tunashukuru kwamba ndugu zetu nchini Filipino wanaendelea kuvumilia, wakimtegemea Mungu wetu, Yehova, ambaye “ni mwenye upendo mwororo sana na mwenye rehema.”—Yakobo 5:11.