Hamia kwenye habari

JULAI 26, 2019
DENMARK

Copenhagen, Denmark—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe!”

  • Tarehe: Julai 19-21, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa Brøndby na ukumbi wa Brøndby Hallen, huko Copenhagen, Denmark

  • Lugha ya Programu: Kidenishi, Lugha ya Ishara ya Kidenishi, Kiingereza, Lugha ya Iceland, Lugha ya Ishara ya Kinorwei, Lugha ya Ishara ya Kiswedi

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 26,409

  • Idadi ya Waliobatizwa: 141

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 7,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Brazili, Amerika ya Kati, Ulaya ya Kati, Kolombia, Jamhuri ya Dominika, Finland, Georgia, India, Japani, Poland, Marekani

  • Mambo Yaliyoonwa : Christian Tidemand Andersen, mratibu wa matamasha wa uwanja wa Brøndby, alisema: “Tulianza kupanga Kusanyiko la Kimataifa la Mashahidi wa Yehova mwaka mmoja na nusu uliopita na kumekuwa na mazungumzo mazuri kati yetu. Kuheshimu na kuelewa changamoto za kila pande kuhusiana na tukio kubwa kama hili, kulifanya mipango yote ikamilishwe kwa njia yenye manufaa. Ni mara chache tunafanya kazi na watu waliojipanga ambao wamefikiria hata mambo madogo-madogo. Katika siku za kusanyiko, tulivutiwa kuona jinsi wajitoleaji walivyofanya kazi kwa bidii kuanzia asubuhi hadi usiku, na wote walikuwa na mtazamo mzuri na tabasamu katika nyuso zao. Tumefurahi sana kuwa sehemu ya tukio hilo, na tungependa kushukuru sana kwa ushirikiano ulioonyeshwa na Halmashauri ya Kusanyiko na wajitoleaji wote. Tunatumaini kuwaona tena nyinyi na wageni wenu hapa katika uwanja wa michezo wa Brøndby.”

 

Wanabetheli waliovaa utepe wa rangi ya njano wakiwakaribisha kwa uchangamfu wajumbe waliotembelea Betheli

Watoto wadogo wakiwa na wazazi wao wakiwakaribisha wajumbe kwenye mkutano wa utumishi

Ndugu na dada wakiingia kusanyikoni katika Uwanja wa Brøndby

Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakipigwa picha wakiwa wamevalia nguo zao za kitamaduni

Akina dada wanaozungumza lugha ya Iceland wakitoa machozi ya furaha wanapopokea nakala zao za Biblia mpya ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo katika lugha ya Iceland

Ndugu Stephen Lett, mshiriki wa Baraza Linaloongoza akitoa hotuba ya mwisho siku ya Ijumaa

Wale wanaotarajia kubatizwa wakisikiliza hotuba mbele ya jukwaa

Baadhi ya ndugu na dada wapya kati ya 141 wakibatizwa

Wamishonari na watumishi wengine wa pekee wakiwapungia mkono ndugu na dada walio uwanjani

Ndugu wakiigiza historia ya kitheokrasi ya nchi za Denmark, Visiwa vya Faroe, Greenland, na Iceland