Hamia kwenye habari

Jumba la Kusanyiko lililo katika Jiji la Recife, katika Jimbo la Pernambuco, nchini Brazili, limepata uharibifu mkubwa

JUNI 10, 2022
BRAZILI

Mafuriko na Mmomonyoko wa Udongo Wasababisha Uharibifu Mkubwa Nchini Brazili

Mafuriko na Mmomonyoko wa Udongo Wasababisha Uharibifu Mkubwa Nchini Brazili

Mvua kubwa iliyoanza Mei 25, 2022 imesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa upande wa kaskazini-mashariki wa nchi ya Brazili. Majimbo ambayo yameharibiwa zaidi ni Alagoas na Pernambuco, na hali ya hatari imetangazwa kwenye miji 42. Zaidi ya watu 145,000 wamelazimika kuhama makazi yao, na watu 129 wamekufa kutokana na mafuriko hayo.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa

  • Wahubiri 3 wamepata majeraha madogo

  • Nyumba 280 zimepata uharibifu mdogo

  • Nyumba 22 zimepata uharibifu mkubwa

  • Majumba 23 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Kusanyiko limepata uharibifu mkubwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada inaandaa mahitaji ya lazima ya kimwili na ya kiroho kwa ajili ya wahubiri zaidi ya 600

  • Jitihada zote za kutoa msaada, zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Tunasali kwamba akina ndugu ‘waendelee kujipatia nguvu katika Bwana’ wanapokabiliana na janga hilo la asili.​—Waefeso 6:10.