Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 16, 2019
AFRIKA KUSINI

Johannesburg, Afrika Kusini—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”

  • Tarehe: Septemba 6-8, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa FNB Johannesburg, Afrika Kusini

  • Lugha za Programu: Kiingereza, Kisesotho, Kizulu

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 58,149

  • Idadi ya Waliobatizwa: 476

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Bolivia, Congo (Kinshasa), Finland, Hong Kong, Hungaria, Israel, Japani, Kenya, Korea, Liberia, Madagaska, Malawi, Marekani, Paraguai, Peru, Uganda, Uingereza, Ulaya ya Kati, Zambia, Zimbabwe

  • Mambo Yaliyoonwa: Wasimamizi wa hifadhi ambayo wajumbe walitembelea inayoitwa Lion and Safari Park, walieleza kwamba hawajawahi kuona watu wa utamaduni na lugha nyingi tofauti-tofauti kadiri hiyo wakishuka kutoka kwenye basi moja bila ubishi au malalamiko. Wasimamizi hao walivutiwa sana na jinsi wageni walivyofuata mwelekezo na kushirikiana na wafanyakazi hivi kwamba wakasema: “Tulifurahi sana kwamba walitutembelea!”

 

Kikundi cha ndugu na dada wenyeji kwenye uwanja wa ndege wakiwakaribisha wajumbe waliowasili nchini Afrika Kusini

Akina dada wanne, wawili wenyeji na wajumbe wawili, wakisambaza mialiko ya kusanyiko katika huduma

Wahudhuriaji wa kusanyiko wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni wakisimama ili kupigwa picha

Ndugu na dada wakitabasamu na kupiga makofi wakati wa kusanyiko

Mmoja kati ya watu 476 waliobatizwa

Ndugu Anthony Morris, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akiwasalimu akina ndugu na dada wakati wa mapumziko

Watumishi wa wakati wote kutoka nchi nyingine wakitambulishwa mbele ya wahudhuriaji, siku ya mwisho ya kusanyiko

Picha ya akina dada watatu baada ya programu ya kusanyiko

Kwaya iliyovalia mavazi yenye kupendeza ya Kiafrika ikiwatumbuiza wasikilizaji wakati wa tafrija ya jioni