Hamia kwenye habari

Jumba la Ufalme lililoathiriwa na mafuriko (kushoto) na nyumba ya ndugu yetu (kulia)

JUNI 10, 2019
PARAGUAI

Mafuriko Yakumba Nchi ya Paraguai

Tangu mwishoni mwa Aprili 2019, mvua kubwa zimekumba nchi ya Paraguai na kusababisha mafuriko yenye uharibifu mkubwa katika maeneo ambayo Mto Paraguai unapita. Watu sita hivi wamekufa kutokana na mafuriko hayo.

Ofisi ya tawi ya Paraguai imeripoti kwamba janga hilo limeathiri ndugu 137 katika majiji kadhaa. Katika mji mkuu wa Asunción, mafuriko yaliharibu ukuta wa Jumba la Ufalme lililotumiwa kufanyia Shule ya Waeneza-Injili wa Ufalme. Inapendeza kujua kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Ofisi ya tawi imetuma msaada wa chakula, maji, na mahitaji mengine ya msingi kwa ndugu na dada walioathiriwa. Kwa kuwa mafuriko bado yanaendelea, ofisi ya tawi inafuatilia kwa ukaribu hali hiyo na itaendelea kuwategemeza ndugu na dada kulingana na uhitaji wao, iwe ni uhitaji wa kimwili au wa kiroho.

Tunasali kwa ajili ya ndugu na dada zetu walioathiriwa na mafuriko nchini Paraguai. Tunajua kwamba Yehova atakuwa “ngome” yao katika kipindi hiki kigumu.—Zaburi 31:2.