Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 28, 2018
JAPANI

Tetemeko la Ardhi Latokea Hokkaido, Japani

Tetemeko la Ardhi Latokea Hokkaido, Japani

Septemba 6, 2018 tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 6.7 lilitokea kule Hokkaido, kisiwa cha kaskazini cha Japani. Tetemeko hilo lilisababisha vifo vya watu 41 na kukatiza umeme katika sehemu kubwa sana, na hivyo kuzuia usafiri wa umma na mawasiliano katika kisiwa hicho.

Ofisi ya tawi ya Japani inaripoti kwamba ingawa hakuna yeyote kati ya ndugu na dada zetu waliokufa, saba walijeruhiwa wakati wa tetemeko hilo. Jumla ya nyumba 100 za Mashahidi na Majumba 4 ya Ufalme yaliharibiwa.

Chini ya uongozi wa ofisi ya tawi, wahubiri waliwapelekea ndugu walioathiriwa chakula, maji na mahitaji mengine punde tu baada ya tetemeko hilo. Halmashauri ya Kutoa Msaada Wakati wa Misiba iliundwa ili kushughulikia utoaji wa misaada kwa muda mrefu zaidi.

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwapa amani ya akili na moyoni ndugu na dada zetu walioathiriwa.—Wafilipi 4:6, 7.