Hamia kwenye habari

Poromoko la ardhi katika jimbo la Fukushima baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Japani kaskazini-mashariki

FEBRUARI 23, 2021
JAPANI

Tetemeko la Ardhi Lapiga Japani Kaskazini-Mashariki

Tetemeko la Ardhi Lapiga Japani Kaskazini-Mashariki

Mahali

Kaskazini-mashariki mwa Japani, hasa majimbo ya Fukushima na Miyagi

Janga

  • Februari 13, 2021, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.3 lilisababisha ukosefu wa umeme na maji katika maeneo fulani. Uharibifu mkubwa ulitokea katika maeneo yaleyale yaliyokuwa yamekumbwa na tetemeko kubwa lenye kipimo cha 9.0 mnamo 2011

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 11 walijeruhiwa

  • Ndugu wengi walikosa umeme na maji kwa muda fulani

Uharibifu wa mali

  • Majumba 10 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

  • Nyumba 205 zilipata uharibifu mdogo

  • Nyumba 13 zilipata uharibifu mkubwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa wanawaandalia wahubiri msaada wa kiroho kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

  • Wawakilishi wa Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi pamoja na wajitoleaji wa idara hiyo wanachunguza kiwango cha uharibifu katika kila Jumba la Ufalme na nyumba za akina ndugu

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwaimarisha walioathiriwa na tetemeko hilo la ardhi.—Wafilipi 4:13.