Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

DESEMBA 13, 2016
VISIWA VYA SOLOMON

Tetemeko la Nchi Latishia Kutokeza Tsunami katika Visiwa vya Solomon

Tetemeko la Nchi Latishia Kutokeza Tsunami katika Visiwa vya Solomon

Mnamo Desemba 9, 2016, tetemeko la nchi lenye kipimo cha 7.8 lilitokea katika pwani ya Visiwa vya Solomon, na kusababisha matetemeko mengine madogo yaliyosababisha mawimbi madogo ya tsunami. Hakuna Shahidi yeyote katika eneo hilo aliyekufa au kujeruhiwa, na hakuna jengo lolote la Mashahidi lililoharibiwa vibaya. Hata hivyo, kwa kuwa majengo ya ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova yako katika mji mkuu, Honiara, ambao uko karibu na pwani, ofisi ya tawi iliwahamisha wafanyakazi wake na kuwapeleka katika eneo lililoinuka kulingana na maonyo yaliyotolewa na Kituo cha Pacific Tsunami Warning. Kwa kuwa sasa hakuna hatari, wafanyakazi wote wamerudi kwenye ofisi ya tawi, na kazi inaendelea kama kawaida.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Visiwa vya Solomon: Lency Lamani, +677-22241