Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

JUNI 27, 2017
UINGEREZA

Mashahidi Watoa Msaada Baada ya Moto Kuteketeza Jengo Jijini London

Mashahidi Watoa Msaada Baada ya Moto Kuteketeza Jengo Jijini London

Mashahidi wa Yehova wanawasaidia watu walioathiriwa na moto kwenye jengo la Grenfell Tower, jengo lenye orofa 24 eneo la Kensington Kaskazini, London, usiku sana Juni 14, 2017. Wenye mamlaka wanasema kwamba watu 79 hivi walikufa.

Mashahidi wanne waliokolewa kutoka katika jengo hilo. Wawili kati yao ni wakaaji wa jengo hilo la Grenfell Tower. Inafurahisha kujua kwamba hawakuumia, ingawa nyumba zao ni kati ya zile zilizoteketezwa kabisa. Mashahidi wanaoishi karibu na jengo hilo lililoteketezwa waliwaandalia wao na familia zao chakula, mavazi, na pesa. Pia, Mashahidi wanawafariji kiroho wakaaji wa Kensington wanaoomboleza.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Uingereza: Andrew Schofield, simu +44-20-8906-2211