Mashahidi wa Yehova wanajitahidi kuwasaidia waabudu wenzao na vilevile wengine walioathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua zilizoanza Mei 26, ambayo yaliharibu eneo la kusini na magharibi ya Sri Lanka. Ripoti zinaonyesha kwamba watu zaidi ya 200 wamekufa na wengine zaidi ya 77,000 wamehama makwao.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Sri Lanka ilianzisha vikosi viwili vya kutoa msaada ili kutunza mahitaji ya lazima ya Mashahidi zaidi ya 100 walioathiriwa na mafuriko, msaada huo ulitia ndani kuwapa chakula na mahali pa kulala. Hakuna Mashahidi waliokufa katika majanga hayo.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa msaada kutoka makao makuu jijini New York, wakitumia michango iliyotolewa kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ya ulimwenguni pote.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Sri Lanka: Nidhu David, simu +94-11-2930-444