Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

SEPTEMBA 25, 2017
PUERTO RIKO

Habari za Karibuni Kuhusu Puerto Riko Baada ya Kimbunga Maria

Habari za Karibuni Kuhusu Puerto Riko Baada ya Kimbunga Maria

Kufikia Septemba 25, 2017, tulikuwa tumepata habari kutoka kwa waangalizi 15 kati ya waangalizi 19 wanaotumikia nchini Puerto Riko kwamba ni ndugu mmoja tu aliyejeruhiwa kwa sababu ya Kimbunga Maria. Bado hatujapata habari za karibuni kutoka kwa waangalizi wanne wa mzunguko walio upande wa magharibi wa kisiwa hicho kwa kuwa hakuna njia ya kuwasiliana nao. Ndugu kutoka mizunguko ya karibu wamekuwa wakitafuta pikipiki na magari makubwa ili wasafiri upande wa magharibi kuona jinsi hali ilivyo.

Tunaendelea kuwakumbuka ndugu na dada zetu wapendwa katika sala.—Yakobo 5:16.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000