Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

APRILI 28, 2015
NEPAL

Tetemeko Kubwa Nchini Nepal

Tetemeko Kubwa Nchini Nepal

Jumamosi, Aprili 25, 2015, tetemeko la nchi lenye kipimo cha 7.8 lilisababisha uharibifu mkubwa sana Kathmandu, jiji kuu la Nepal. Tetemeko hilo lilifuatwa na matetemeko mengine mengi, baadhi ya hayo yalikuwa na kipimo cha 6.6. Jitihada za kutathmini uharibifu huo zinaendelea, lakini habari za karibuni kutoka ofisi ya Mashahidi wa Yehova ya jijini Kathmandu, zinaripoti kwamba Shahidi mmoja na watoto wake wawili walikufa. Pia, nyumba nyingi za Mashahidi zimeharibiwa. Ofisi ya Mashahidi pia iliharibiwa kidogo. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Japan inashirikiana na ofisi ya Nepal katika jitihada za kutoa msaada.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Japan: Ichiki Matsunaga, simu +81 46 233 0005

Nepal: Reuben Thapaliya, simu +977 9813469616