Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

DESEMBA 20, 2016
MAREKANI

Mashahidi Wauza Uwanja Mkubwa wa 85 Jay Street Ulioko Brooklyn

Mashahidi Wauza Uwanja Mkubwa wa 85 Jay Street Ulioko Brooklyn

Jumanne, Desemba 20, 2016, Mashahidi wa Yehova waliwauzia wawekezaji wa makampuni ya Kushner, CIM Group, na LIVWRK uwanja wa 85 Jay Street. Uwanja huo mkubwa uko kwenye eneo la jiji linalozidi kusitawi huko Dumbo, Brooklyn, na lina ukubwa wa mita 92,903 za mraba zinazoweza kutumiwa kwa ajili ya kazi mbalimbali.

Mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, jengo hilo lilitia ndani majengo kadhaa yaliyokuwa yameharibika. Mashahidi waliponunua eneo hilo, walikusudia kupanua majengo hayo ili yatumiwe kwa ajili ya kazi ya uchapishaji inayozidi kuongezeka. Hata hivyo, Mashahidi waliamua kuhamisha kazi ya kuchapa, kujalidi, na kusafirisha machapisho kutoka Brooklyn hadi kwenye ofisi zao zilizoko Wallkill, New York. Hivi karibuni, Mashahidi walihamisha makao yao makuu ya ulimwenguni pote kutoka Brooklyn hadi Warwick, New York, na kwa miaka kadhaa iliyopita, wamekuwa wakiuza majengo yao yaliyoko katika maeneo ya Brooklyn Heights na Dumbo.

Richard Devine, msemaji wa Mashahidi wa Yehova, anasema hivi: “Majengo kama 85 Jay Street hayapatikani kwa urahisi, hasa ukizingatia ukubwa wake, mahali lilipo, na manufaa yake ya wakati ujao.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000