Novemba 29, 2016, Mashahidi wa Yehova walikamilisha shughuli za kuuza jengo lao la 69 Adams Street, Brooklyn, New York. Jengo hilo lenye mita 7,026 za mraba limejengwa kwenye eneo la Dumbo karibu na bahari na lipo katikati ya daraja la Brooklyn na la Manhattan.

Mwaka wa 1994, Mashahidi wa Yehova walijenga jengo lenye ghorofa nne na walilitumia kama jengo la maegesho na burudani. Jengo hilo lina nafasi 84 za maegesho ambazo zilikuwa zikihudumiwa na lifti mbili za gari.

Richard Devine, msemaji wa Mashahidi wa Yehova, anasema hivi: “Jengo la 69 Adams ni uwanja wenye thamani kubwa sana, si kwa sababu tu liko katika eneo zuri bali pia kwa sababu lina nafasi ya kuliendeleza. Sheria ya ugawaji wa maeneo zinaruhusu jengo hilo liinuliwe kutoka urefu wake wa sasa wa mita 26. Sheria hizo zinaliruhusu lijengwe kufikia urefu wa mita 85 kwenda juu na upana wa mita 14,586 za mraba.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-845-524-3000