Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

DESEMBA 9, 2015
MAREKANI

Mashahidi Wakamilisha Sehemu Kubwa ya Ujenzi wa Makao Makuu Mapya

Mashahidi Wakamilisha Sehemu Kubwa ya Ujenzi wa Makao Makuu Mapya

NEW YORK—Kuanzia Agosti hadi Oktoba 2015, sehemu kubwa ya ujenzi wa makao makuu mapya ya Mashahidi wa Yehova ya Warwick, New York umefanyika, na watu 3,800 walijitolea kila siku kusaidia ujenzi.

Katika kipindi cha upeo wa ujenzi, mabasi 40 hivi yalitumika kuwasafirisha wajitoleaji 3,800 hivi kila siku.

Vyumba vinane vya muda vya kulia chakula vimetumika kwa ajili ya wajitoleaji.

Tangu ujenzi ulipoanza Julai 2013, Mashahidi zaidi ya 18,000 wamesafiri kutoka katika kila jimbo kutia ndani Alaska na Hawaii ili kusaidia kazi ya ujenzi. Kwa kawaida angalau wafanyakazi 400 hadi 500 hufika kila mwisho juma, lakini katika kipindi hicho chenye shughuli nyingi, zaidi ya wafanyakazi 700 walifika. Wajitoleaji wengi walifanya kazi kwa juma moja hadi majuma manne.

Richard Devine, ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi (CPC) wa Warwick anaeleza hivi: “Ikiwa tungetumia maelfu ya wafanyakazi kila siku huenda kungekuwa na msongamano mkubwa katika eneo la kazi. Lakini ili kufanya mambo kwa utaratibu na ufanisi, tuliamua kuunda kikosi cha pili cha wafanyakazi 400 hivi kilichokuwa kikianza kazi saa 9 mchana hadi saa 8 usiku.” Kikosi hicho kimekuwa kikifanya hivyo kuanzia Mei hadi Septemba.

Picha ya mwingilio wa makao makuu ya ulimwenguni pote ya Mashahidi wakati wa machweo ya jua.

Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi inaeleza kwamba ujenzi wa majengo mawili kati ya manne ya makazi utakuwa umekamilika kufikia mwezi wa Januari 2016, kama ilivyokuwa imepangwa mapema. Hata hivyo, Bw. Devine, anaeleza kwamba “kwa sababu ya ushirikiano mkubwa uliopo sehemu kubwa ya ujenzi imekamilika miezi minne kabla ya muda uliokuwa umeratibiwa.” Ujenzi uliobaki wa majengo ya makazi, ofisi, na udumishaji umepangwa kukamilika Septemba 1, 2016.

Makao makuu mapya ya ulimwenguni pote kutoka juu.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000