Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

DESEMBA 7, 2015
MAREKANI

Mashahidi Waanza Kuuza Majengo Brooklyn

Mashahidi Waanza Kuuza Majengo Brooklyn

NEW YORK—Mashahidi wa Yehova wanauza baadhi ya majengo ambayo wanunuzi wengi sana wanayataka ya Dumbo na Brooklyn Heights huko Brooklyn, New York. Kazi ya kutafuta mnunuzi bora imeanza kwa ajili ya jengo la Mtaa wa 85 Jay na jengo la makazi lenye orofa kumi la 124 Columbia Heights imeanza. Pia, eneo la sasa la makao makuu ya ulimwenguni pote la 25/30 Columbia Heights, linauzwa. Maeneo hayo matatu yanauzwa na Idara ya Ununuzi na Uuzaji wa Majengo ya Watchtower (Watchtower Real Estate Office) na hayatarajiwi kuuzwa kwa pamoja.

Akizungumza kuhusu Mtaa wa 85 Jay, wenye ukubwa wa mita 12,542 za mraba, Richard Devine, msemaji mmoja wa Mashahidi wa Yehova, anasema hivi: “Eneo hilo ni kubwa katika ujirani unaovutia wa Dumbo na linaweza kufanyiwa mambo mengi kuliendeleza.”

Majengo kwenye Mtaa wa Jay 85 yako chini ya Daraja la Manhattan katika ujirani unaovutia wa Dumbo.

Jengo la makazi la Mashahidi lenye ukubwa wa mita 14,121 za mraba la 124 Columbia Heights liko kwenye Wilaya ya Kihistoria ya Brooklyn Heights. Bw. Devine anasema hivi: “Ni jengo zuri linalomsaidia mtu kuona mandhari ya kipekee ya Daraja la Brooklyn, Sanamu ya Uhuru (Statue of Liberty), na sehemu ya anga inayopendeza sana ya kusini mwa Manhattan.”

Eneo la 124 Columbia Heights lililopo kwenye ujirani wa eneo la kihistoria la Brooklyn Heights.

Makao makuu ya ulimwenguni pote ya Mashahidi wa Yehova yamekuwa kwenye eneo la 25/30 Columbia Heights (tazama picha juu) kwa makumi ya miaka na watu wengi wanaoishi New York huyafahamu kwa maandishi yenye maneno Watchtower na saa iliyo juu yake. Makao hayo yako kwenye eneo kubwa lenye zaidi ya mita 68,098 za mraba na ukiwa hapo unaweza kuona Daraja la Brooklyn bila kizuizi.

Akizungumzia mipango ya Mashahidi ya wakati ujao, Bw. Devine anasema, “Kuuza majengo haya ni hatua zinazofuata za kuhamisha makao yetu makuu kwenda Warwick, New York.”

Kwa maelezo zaidi kuhusu majengo hayo, tafadhali tembelea tovuti hii; www.watchtowerbrooklynrealestate.com. Unaweza kufanya mahojiano na kupata picha ukiwasiliana na Ofisi ya Habari za Umma.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000