Maporomoko ya ardhi yenye upana wa kilometa moja na nusu yalifunika nyumba za watu huko Snohomish County, Washington, Marekani, Machi 22, 2014. Wakuu wa serikali katika eneo hilo wanasema kwamba asilimia 90 hivi ya watu hawajulikani walipo na watu 17 wamekufa. Ofisi ya Tawi ya Mashahidi wa Yehova inaripoti kwamba Shahidi mmoja mwanamke ni kati ya wasiojulikana waliopo. Wenzi fulani wa ndoa ambao ni Mashahidi wamempoteza binti yao na kitukuu chao katika maporomoko hayo ya ardhi. Mashahidi wawili walilazimika kuhama nyumba zao; nyumba ya Shahidi mwingine iliharibiwa kabisa. Waangalizi Mashahidi wanawapa msaada na kuwafariji wale walioathiriwa na janga hilo

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000