Agosti 31, 2017, Mashahidi wa Yehova walimaliza mchakato wa kuuza 97 Columbia Heights. Jengo hilo lenye upana wa mita 8,232 za mraba lilikuwa makazi ya Mashahidi waliofanya kazi kwenye makao makuu kwa miaka zaidi ya 30. Zamani lilitumika kama eneo la kihistoria la Hoteli Margaret, linapendeza kwa sababu ukiwa hapo unaweza kuona mandhari nzuri ya East River na Manhattan skyline, linapatikana jirani na eneo la kihistoria la wilaya ya Brooklyn Heights, na paa na bustani zilizo nje ya vyumba vyake. Mapema katika Agosti 11, 2017, Mashahidi pia walikamilisha mchakato wa kuuza jengo lingine lililoko 119 Columbia Heights.

Makao makuu ya Mashahidi wa Yehova sasa yapo Warwick, New York.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000