Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

SEPTEMBA 11, 2017
MAREKANI

Habari za Karibuni Kuhusu Kimbunga Irma

Habari za Karibuni Kuhusu Kimbunga Irma

Tumeanza kupata habari kuhusu ndugu na dada zetu huko Karibea na kusini mashariki ya Marekani baada ya Kimbunga Irma.

Inasikitisha kwamba ndugu mmoja aliyezeeka huko Florida na dada mmoja huko Georgia walikufa wakati wa kuhamishwa. Pia, ndugu wawili walijeruhiwa huko Tortola, kisiwa kikubwa zaidi kati ya Visiwa vya Virgin vya Uingereza. Kotekote katika Karibea, nyumba zaidi ya 40 zimeharibiwa na ndugu 40 hivi wamelazimika kuhama nyumba zao. Uchunguzi bado unaendelea kadiri ndugu wanavyoweza kuingia kwenye maeneo yaliyoathiriwa.

Tunaomboleza na wale waliofiwa na wapendwa wao na tunawasikitikia wengi ambao wameathiriwa na dhoruba. Tunaendelea kutegemea faraja ambayo Yehova anaandaa kupitia kutaniko.—1 Wathesalonike 3:7.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000