Ijumaa, Desemba 14, 2012, mtu fulani alifyatua risasi katika shule ya watoto wachanga huko Newtown, Connecticut. Vyombo vya habari vinaripoti kwamba zaidi ya watu 27 waliuawa, kutia ndani mtu huyo aliyefyatua risasi na watoto 20. Ripoti za sasa zinasema kwamba angalau watoto wawili Mashahidi walikuwepo katika shule hiyo risasi zilipofyatuliwa lakini hawakujeruhiwa. Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo wanasaidia familia zilizoathiriwa na msiba huo na pia wanawapa watu katika eneo hilo faraja ya kiroho.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J.R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, +1 718 560 5000