Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

NOVEMBA 7, 2012
MAREKANI

Mashahidi wa Yehova Wauza Jengo Lililokuwa Hoteli ya Bossert

Mashahidi wa Yehova Wauza Jengo Lililokuwa Hoteli ya Bossert

Mashahidi wa Yehova wameuza jengo lililokuwa Hoteli ya Bossert inayopatikana katika Barabara ya 98 Montague, katika eneo la kihistoria la Brooklyn Heights huko New York City. Jengo hilo limenunuliwa na David Bistricer wa kampuni ya Clipper Equity and the Chetrit Group. Katika mwaka wa 1983 Mashahidi walianza kurekebisha jengo hilo lote kupatana na viwango vya wilaya vya Kuhifadhi Maeneo ya Kihistoria, na wamepata tuzo nyingi kwa sababu ya kazi yao. David Semonian, msemaji wa Mashahidi alisema hivi: “Tulifurahia kurekebisha jengo hilo la Bossert kwa miaka 25 ambayo imepita. Ni jengo maridadi sana, na limekuwa na sehemu muhimu katika historia yetu.”

Media Contact: David Semonian, Office of Public Information, tel. +1 718 560 5000