Katikati ya Septemba, mvua kubwa ilinyesha katika jimbo la Colorado, Marekani, na kusababisha mafuriko yaliyofanya barabara zifungwe, yakaharibu nyumba, na kusababisha vifo vya angalau watu 8. Ripoti zinaonyesha kwamba hakuna Shahidi wa Yehova katika eneo hilo ambaye alikufa au kujeruhiwa. Hata hivyo, karibu familia 70 za Mashahidi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi walihamishwa kutoka nyumbani kwao. Wazee wa makutaniko katika maeneo yaliyoathiriwa wanashughulikia mahitaji ya lazima ya familia zilizohamishwa, wakiwasaidia kupokea makao ya muda.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000