Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

OKTOBA 26, 2016
MAREKANI

Mashahidi Watangaza Kuuza 97 Columbia Heights

Mashahidi Watangaza Kuuza 97 Columbia Heights

Kwa miaka mingi, hoteli maridadi iliyoitwa Hotel Margaret ilikuwa jengo refu zaidi Brooklyn.

NEW YORK—Jumatano, Oktoba 26, 2016, Mashahidi wa Yehova walitangaza kwamba jengo lao la 97 Columbia Heights huko Brooklyn, New York, lilikuwa likiuzwa. Jengo hilo la makazi lenye orofa 11, ambapo mtu anaweza kuona maeneo yenye kupendeza ya East River na majengo marefu ya Manhattan, liko upande wa kaskazini wa wilaya maridadi na ya kihistoria ya Brooklyn Heights.

97 Columbia Heights ilijengwa kwa kutumia shaba, vigae maridadi, na madirisha makubwa ya pembeni kama tu Hotel Margaret.

Jengo hilo limejengwa mahali ambapo hoteli iliyoitwa Hotel Margaret, iliyoteketea mwaka wa 1980, ilikuwa imejengwa. Mchora-ramani Stanton Eckstut alipewa kazi ya kuchora ramani ya ujenzi ya jengo jipya la makao, mchoro uliotia ndani mambo mbalimbali yaliyokuwepo katika hoteli ya awali kama vile ujenzi wa kutumia shaba, vigae maridadi, na madirisha makubwa ya pembeni. Mwaka wa 1986, ujenzi ulipokuwa ukiendelea, jengo hilo jipya liliuzwa kwa Mashahidi, na limekuwa likitumiwa kama makazi ya wafanyakazi wa makao makuu yao. David A. Semonian, msemaji wa Mashahidi wa Yehova katika makao yao makuu, anaeleza hivi: “Kwa miaka 30 iliyopita, mamia ya watu wanaofanya kazi katika makao makuu waliliona jengo la 97 Columbia Heights kuwa makao yao. Mwonekano wenye kupendeza wa jengo hilo na mahali lilipojengwa unalifanya liwe sehemu nzuri ya kuishi.”

Jengo hilo lenye mita za mraba 8,232 lina vyumba 97 vya makazi. Baadhi yake zina veranda na nyingine zina veranda kwenye paa. Jengo hilo pia lina gereji la ndani lililo na nafasi 30 za kuegesha magari ambalo linafikika kwa urahisi kupitia mwingilio wa kibinafsi unaopatikana Orange Street.

Mr. Semonian anasema: “Wafanyakazi wetu na ofisi zetu zimekuwa zikihamia makao makuu mapya huko Warwick, New York, ambayo yalianza kutumiwa rasmi Septemba 1, 2016. Kuuzwa kwa 97 Columbia Heights ndiyo hatua ya karibuni zaidi katika mpango huo wa kuhama.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-718-560-5000