Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

MEI 17, 2017
MAREKANI

Mashahidi Wakamilisha Mkataba wa Kuuza 107 Columbia Heights, Makao Makuu ya Zamani Mjini Brooklyn

Mashahidi Wakamilisha Mkataba wa Kuuza 107 Columbia Heights, Makao Makuu ya Zamani Mjini Brooklyn

NEW YORK—Mei 9, 2017, Mashahidi wa Yehova na shirika linaloshirikiana na Clipper Realty walikamilisha mkataba wa kuuza 107 Columbia Heights, iliyo kwenye Wilaya ya Kihistoria ya Brooklyn Heights jijini New York. Tangu mwaka wa 1960, jengo hilo limetumiwa kwa ajili ya makazi ya Mashahidi wanaofanya kazi kwenye makao makuu.

Jengo hilo lenye orofa 11, kwenye eneo lenye ukubwa wa mita 14,312 za mraba liko kando ya eneo lenye kupendeza la Brooklyn Heights. Ina ua wenye bustani maridadi, chemchemi na eneo unaloweza kuona daraja la Brooklyn, Mto East, na Manhattan.

Picha ya bustani na chemchemi ya 107 Columbia Heights.

“Tulifurahi kuona majirani wetu, hasa familia changa, wakithamini eneo la 107 Columbia Heights walipopita au kufurahia chemchemi yetu na mwingilio wa bustani,” anakumbuka David A. Semonian, msemaji wa Mashahidi kwenye makao makuu mapya Warwick, New York. “Eneo hilo lilitufaa kwa miaka zaidi ya 50 na lilikuwa mojawapo ya sehemu muhimu kwenye eneo la Brooklyn Heights.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000