Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

JANUARI 14, 2015
KROATIA

Mashahidi Wapata Itikio Zuri Katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Nchini Kroatia

Mashahidi Wapata Itikio Zuri Katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Nchini Kroatia

ZAGREB, Kroatia—Novemba 11-16, 2014, ilikuwa mara ya kwanza kwa Mashahidi wa Yehova kushiriki katika maonyesho ya kimataifa yanayojulikana kama Interliber International Book and Teaching Appliances Fair. Tukio hilo la kila mwaka huwa na mamia ya washiriki wanaotoka katika nyanja mbalimbali za uchapishaji na elimu na ni moja ya maonyesho bora zaidi ya kibiashara nchini Kroatia. Mwaka huu ulikuwa na kilele kipya cha wahudhuriaji 130,000.

Rais wa Jamhuri ya Kroatia, Dakt. Ivo Josipoviæ, akitembelea maonyesho ya Mashahidi na kuchagua machapisho.

Miongoni mwa wageni waliotembelea kibanda cha maonyesho cha Mashahidi ni Rais wa Jamhuri ya Kroatia, Dakt. Ivo Josipoviæ. Rais Josipoviæ aliwasalimu Mashahidi na kuchagua baadhi ya machapisho yanayohusu sayansi na Biblia yenye kichwa Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai, Uhai—Ulitokana na Muumba?, na Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?

“Kona ya watoto” ilikuwa na machapisho yaliyokusudiwa kwa ajili ya watoto na wazazi, na video za vibonzo kutoka Tovuti ya jw.org.

Sehemu ya maonyesho ya Mashahidi iliyopendwa zaidi ni “kona ya watoto,” ambapo wageni walitazama video za vibonzo kutoka kwenye Tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova, jw.org, zinazokusudiwa kuwafundisha watoto masomo mbalimbali kutoka katika Biblia. Wageni wengi walichagua vitabu viwili vyenye kichwa Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, vinavyotoa mwongozo mzuri kwa vijana na wazazi.

Josip Lioviæ, msemaji wa Mashahidi wa Yehova nchini Kroatia, alieleza hivi: “Tumefurahia sana itikio zuri tulilopata kwenye maonyesho haya ya Interliber. Maonyesho yetu yalifanikiwa sana kuliko tulivyotazamia, na wageni walichukua zaidi ya machapisho 7,500. Tunatazamia kwa hamu kuwaonyesha wageni machapisho yetu kwa mara nyingine tena mwaka ujao.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Croatia: Josip Lioviæ, simu +385 91 5336 511