Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

NOVEMBA 4, 2016
KAMERUN

Aksidenti Mbaya ya Garimoshi Nchini Kamerun

Aksidenti Mbaya ya Garimoshi Nchini Kamerun

Asubuhi ya Oktoba 21, 2016, garimoshi lililokuwa likisafiri kuelekea jiji la bandarini la Douala, Kamerun, liliacha reli karibu na mji wa Eseka, kilomita 120 hivi kutoka mji mkuu, Yaoundé. Watu zaidi ya 600 walijeruhiwa katika aksidenti hiyo, na wengine zaidi ya 70 walikufa.

Kati ya wale waliojeruhiwa, kumi na sita walikuwa Mashahidi wa Yehova. Isitoshe, Shahidi wa Yehova, mwenye umri wa miaka 65, ambaye alikuwa mzee wa kutaniko jijini Douala, alikufa katika aksidenti hiyo. Tunasikitishwa sana na kifo cha mwabudu mwenzetu na pia hali ngumu ambayo waathiriwa wote pamoja na familia zao wanapitia.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-718-560-5000

Kamerun: Gilles Mba, 237-6996-30727