Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

APRILI 29, 2016
JAPANI

Matetemeko ya Ardhi Nchini Japani

Matetemeko ya Ardhi Nchini Japani

Aprili 14 na 16, 2016, matetemeko mawili makubwa ya ardhi yalitikisa kisiwa cha Kyushu kilichopo kusini mwa Japani. Tetemeko la kwanza lilikuwa na kipimo cha 6.5, na la pili lilikuwa na kipimo cha 7.3. Kulikuwa na matetemeko mengi madogo madogo yaliyofuata baada ya tetemeko hilo kubwa. Kuna zaidi ya makutaniko 70 ya Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo lililoathiriwa, lakini hakuna hata Shahidi mmoja aliyekufa wala kujeruhiwa vibaya na janga hilo. Hata hivyo, makazi zaidi ya 70 ya Mashahidi yameharibika na 17 yamebomoka. Kwa kuwa matetemeko madogo madogo yanaendelea, zaidi Mashahidi 400 wamehama kutoka katika makazi yao na kwenda kwenye Majumba ya Ufalme, au majengo ya ibada, ambapo wanapata chakula na makazi. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Japani imepanga halmashauri ya kutoa msaada yenye wajitoleaji wenye uzoefu wa kujenga ili kuwahudumia walioathiriwa na tetemeko hilo.

Wanahabari wanaweza kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Japani: Ichiki Matsunaga, simu +81 46 233 0005