Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Italia

MEI 23, 2018

Chuo Kikuu cha Padua Kimefanya Kongamano la Kihistoria la Kuzungumzia Maendeleo ya Matibabu Yasiyohusisha Damu

Kwa muda fulani, ilionekana kwamba kumtia mgonjwa damu mishipani hakuna madhara yoyote na ndiyo mbinu inayoweza kuokoa uhai wakati wa matatizo makubwa ya kiafya au wakati wa upasuaji tata. Lakini wasemaji wengi katika kongamano hilo walipinga wazo hilo.

MEI 23, 2018

Mahojiano na Profesa Antonio D. Pinna, M.D.

“Kwa kweli, sidhani daktari anapaswa kumtendea mgonjwa kwa njia tofauti kwa msingi wa dini. Kwa mfano, kuna wagonjwa ambao si Mashahidi wa Yehova na bado hawataki kutiwa damu mishipani.”

MEI 23, 2018

Mahojiano na Luca P. Weltert, M.D.

“Watu hawatiwi damu sana mishipani, na si wagonjwa Mashahidi tu, bali wagonjwa ulimwenguni pote, kwa sababu uthibitisho unaonyesha kwamba kutotia damu kunakuwa na matokeo mazuri zaidi.”