Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

JUNI 26, 2017
GUATEMALA

Tetemeko Kubwa Karibu na Mpaka wa Guatemala na Mexico

Tetemeko Kubwa Karibu na Mpaka wa Guatemala na Mexico

 

Mashahidi wa Yehova wanawasaidia walioathiriwa na tetemeko kubwa la nchi, ambalo lilipiga eneo la magharibi la Guatemala karibu na mpaka wa Mexico siku ya Jumatano, Juni 14, 2017. Kulingana na habari za karibuni, tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.9 liliwaua watu watano na kusababisha maporomoko kadhaa ya ardhi.

Hakuna Mashahidi wa Yehova walioumia au kufa katika maeneo yaliyoathiriwa. Hata hivyo, majengo 11 ya ibada na nyumba 17 zilihitaji kurekebishwa. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova ya Amerika ya Kati, iliyo Mexico City, imeanzisha halmashauri tatu za kutoa msaada nchini Guatemala ili kukagua madhara yaliyosababishwa na kuharakisha kazi ya kutoa msaada.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linategemeza kazi ya kutoa msaada kutoka makao yao makuu, wakitumia pesa zilizotolewa mchango katika kazi yao ya ulimwenguni pote.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52-555-133-3048

Guatemala: Juan Carlos Rodas, simu +502-5967-6015