Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

AGOSTI 23, 2017
FILIPINO

Moto Wateketeza Nyumba Nyingi Nchini Filipino

Moto Wateketeza Nyumba Nyingi Nchini Filipino

Asubuhi Agosti 5, 2017, moto mbaya sana ulitokea katika eneo la Agdao, katika Jiji la Davao, lililoko kwenye pwani ya Kisiwa cha Mindanao, kusini mwa Filipino.

Ingawa hakuna yeyote kati ya Mashahidi wa Yehova aliyejeruhiwa, nyumba za familia 13 ziliathiriwa vibaya na moto huo kwa hiyo, 29 kati yao wakaachwa bila makao. Mashahidi wenzao wamewakaribisha waathiriwa wa moto huo nyumbani kwao. Ofisi ya Tawi ya Mashahidi wa Yehova iliyoko Manila imeweka rasmi halmashauri ya kutoa msaada ili isimamie kazi ya kugawa msaada.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa msaada kutoka kwenye makao yao makuu, wakitumia michango iliyotolewa kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ya Mashahidi ya inayofanywa ulimwenguni pote.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Filipino: Dean Jacek, +63-2-224-4444