Aprili 16, 2016 tetemeko la kipimo cha 7.8 lilikumba pwani ya bahari ya Pasifiki nchini Ekuado. Tetemeko hilo pamoja na mengine madogo madogo yaliyofuata yamesababisha uharibifu mkubwa na kuua watu zaidi ya 650. Ingawa majengo ya ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Ekuado hayakuathiriwa wakati wa tetemeko hilo, nyumba nyingi za Mashahidi zimebomoka. Ripoti ya hivi karibuni imethibitisha kwamba Shahidi wa Yehova mmoja amekufa kutokana na tetemeko hilo. Mashahidi wametuma magari yenye vyakula na maji ya kunywa kwenye eneo lililoathiriwa. Pia, halmashauri mbili za kutoa msaada zimetumwa haraka na ofisi ya tawi ili kutoa msaada, nazo zimeanzisha vituo viwili vya kutoa msaada, kimoja katika jiji la Pedernales na kingine jijini Manta. Isitoshe, wawakilishi wanne kutoka ofisi ya tawi walitembelea eneo lililoathiriwa ili kuwapa faraja ya kiroho waathirika wa janga hilo.

Wanahabari wanaweza kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Ekuado: Marco Brito, simu +593 98 488 8580