Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

FEBRUARI 15, 2013
AUSTRALIA

Mashahidi wa Yehova Wasaidia Watu Walioathiriwa na Mafuriko Nchini Australia

Mashahidi wa Yehova Wasaidia Watu Walioathiriwa na Mafuriko Nchini Australia

SYDNEY—Australia mashariki ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga cha kitropiki kinachoitwa Oswald ambacho kilisababisha dhoruba kali, mawimbi makubwa, na mvua kubwa katika eneo la Queensland na kaskazini mwa New South Wales. Karibu watu wanne wamekufa, na zaidi ya watu 1,000 wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao. Jiji la Bundaberg, lililo pwani ya kati ya Queensland ndilo hasa lililopigwa zaidi na dhoruba hiyo, na si tu kwamba lilikumbwa na mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya karne moja, bali pia lilikumbwa na vimbunga vitano.

Ofisi ya Tawi ya Mashahidi wa Yehova iliyo jijini Sydney inaripoti kwamba hakuna Mashahidi waliokufa au kujeruhiwa. Hata hivyo, karibu nyumba 53 za Mashahidi katika jiji la Bundaberg ziliharibiwa na kuacha zaidi ya Mashahidi 70 bila makao. Wale waliohamishwa, ambao baadhi yao waliokolewa na Helikopta, wamepewa hifadhi na jirani zao au Mashahidi wenzao walio katika eneo hilo.

Wazee Wakristo katika eneo hilo waliunda halmashauri ya kutoa misaada ili kupanga jitihada za kutoa msaada. Pia, katika eneo la Bundaberg, zaidi ya Mashahidi 250 walijitolea ili kusaidia, baadhi yao hata walisafiri umbali wa zaidi ya kilomita 160 ili kuwasaidia waathiriwa.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu. +1 718 560 5000

Australia: Donald MacLean, simu. +61 2 9829 5600